Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, June 20, 2013

Prof Lipumba mgeni rasmi miaka `13 ya Kikosi cha Mizinga


http://sphotos-a.ak.fbcdn.net/hphotos-ak-ash3/p480x480/712_467874856634160_1616825647_n.jpg
Kiongozi wa Kikosi cha Mizinga, Karama Masoud 'Kalapina'
 MWENYEKITI wa Chama cha CUF, Prof Ibrahim Lipumba anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika onyesho la maadhimisho la miaka 13 ya Kikosi cha Mizinga zinazotarajiwa kufanyika kesho kwenye ukumbi wa Msasani Club, jijini Dar es Salaam.
Kiongozi wa Kikosi, Karama Masoud 'Kalapina' aliiambia MICHARAZO kwamba, Prof Lipumba ndiye atakayekuwa mgeni rasmi baada ya mipango ya awali kumualika Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azan kushindikana kumpaka kwa kuwaomba udhuru.
Kalapina alisema maandalizi ya onyesho hilo ambalo mashabiki watalazimika kulipa Buku 5 tu mlangoni, yamekamilika ikiwemo kuongezeka kwa idadi ya wasanii na makundi yatakayowasindikiza katika onyesho hilo ambalo litaambatana na maonyesho mbalimbali yenye asili ya utamaduni wa Hip hop.
"Maandalizi ya onyesho la Kikosi cha Mizinga yamekamilika ikiwemo kutarajiwa Mwenyekiti wa Kitaifa wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba kuwa mgeni rasmi baada ya kumkosa Mhe. Idd Azan, pia burudani zimeongeza zaidi katika kunogesha miaka hiyo 13," alisema Kalapina. 
Mkali huyo ambaye pia ni mwanaharakati na mwanasiasa alisema baadhi ya wasanii watakaoshiriki kupigwa mizinga 21 ya Kikosi kesho ni Afande Sele, Young Killer, Manzese Crew, Stereo, Kala Jeremiah, LWP, Mansu-Lee, Gangwe Mob  wakiwa na Inspekta Harun na wengine wakiwamo Kikosi cha Mizinga chenyewe.
Shughuli nyingine zitakazoambatana na onyesho hilo ni maonyesho ya uchoraji na kupaka rangi, mitindi ya nguo na mavazi, kucheza break dance na utoaji wa tuzo kwa watu na asasi zilizosaidia Kikosi cha Mizinga kufika hapo ilipo ikiwa inatimiza miaka hiyo 13 tangu kuzaliwa kwake.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...