Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, September 21, 2013

MHE. LUKUVI ATEMBELEA KIWANDA CHA MAJI CHA DEW DROP KILICHOPO SUMBAWANGA MKOANI RUKWA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi akikagua kiwanda cha maji cha Dew Drop kinachomilikiwa na muwekezaji wa ndani Ndugu Aziz Tawaqal alipokuwa ziarani Mkoani Rukwa tarehe 18 Sept 2013. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na Katibu Tawala Mkoa huo Alhaj Salum Mohammed Chima.
Kiwanda cha kisasa cha Dew Drop chenye uwezo wa kuzalisha maji lita 6,000 kwa saa yakiwa na ubora wa hali ya juu. Maji hayo huzalishwa katika hali ya usafi na hayaongezwi  kemikali yeyote ambapo husafishwa kupitia "Sand Filters", "Activated Coal" na teknolojia ya "UV Light".
Mkurugenzi wa Kampuni ya Vinywaji ya Dew Drop Aziz Tawaqal akitoa maelekezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi alipofika kiwandani hapo kujionea shughuli mbalimbali za muwekezaji huyo ikiwemo kiwanda cha unga cha Energy Milling.  
Waziri Lukuvi akipokea maelezo ya Maji ya Dew Drop kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Vinywaji ya Dew Drop Aziz Tawaqal, Waziri huyo aliyasifia maji hayo na kusema kuwa ameyanywa na ni mazuri sana ukilinganisha na maji mengine yanayozalishwa hapa nchini.(Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa...rukwareview.blogspot.com)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...