Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, February 24, 2014

Nyamwela afyatua mpya na Tundaman



MNENGUAJI kiongozi wa bendi ya Extra Bongo, Mussa Hassan 'Super Nyamwela' amefyatua wimbo mpya uitwao 'Nyengele' akimshirikisha nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Tundaman ikiwa ni maandalizi yake ya kupakua albamu yake mpya na ya tatu.
Akizungumza na MICHARAZO, Super Nyamwela alisema wimbo huo ambao ni wa nne katika maandalizi ya albamu hiyo baada ya 'Duvele Duvele', na Maneno Maneno ameurekodia katika studio za C9 Records na anatarajia kuachia wiki ijayo.
Nyamwela alisema katika wimbo huo kama ulivyo 'Duvele Duvele' na 'Tumechete'  umepigwa kiasili kwa ajili ya kuleta vionjo tofauti na kutamba kuwa utakuwa funika bovu kwa namna Tundaman alivyompiga tafu.
"Nipo katika maandalizi ya mwisho ya kuachia audio na video ya wimbo wangu mpya uitwao 'Nyengele' ambao nimeuimba na Tundaman ikiwa ni maandalizi kutoa albamu yangu ya tatu baada ya 'Master of the Tample' na 'Afrika Kilomondo', " alisema Nyamwela.
Nyamwela alisema amepanga ndani ya mwaka huu albamu hiyo ya tatu itakuwa imekamilika na pia itafanyiwa uzinduzi , japo hajajua itafanyika mwezi gani na ukumbi gani.
"Nataka nikamilishe nyimbo zote audio na video kabla ya kuizindua rasmi," alisema Nyawela.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...