Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, March 14, 2014

RIDHIWANI ARUDISHA FOMU ZA UBUNGE CHALINZE



 MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Ridhiwani Kikwete leo amerudisha fomu ya kugombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi, akisindikizwa na washindani wake katika kura za maoni, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ramadhan Maneno pamoja na Imani Madega. 
 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Ridhiwani Kikwete akiwa ameambatana na  washindani wake katika kura za maoni, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ramadhan Maneno pamoja na Imani Madega wakifurahia jambo. 
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Ridhiwani Kikwete akiwa ameambatana na  washindani wake katika kura za maoni, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ramadhan Maneno pamoja na Imani Madega na wadau wengine akielekea kurejesha fomu.
 Baadhi ya Wanahabari wakishuhudia tukio la Urudishwaji fomu wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi mapema leo.

===========  ======== ======
Ridhiwani arudisha fomu za Ubunge Chalinze.

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Ridhiwani Kikwete leo amerudisha fomu ya kugombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi.

Akisindikizwa na washindani wake katika kura za maoni, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ramadhan Maneno pamoja na Imani Madega, Ridhiwani aliwashukuru wana CCM na wakazi wa Chalinze kwa ujumla kwa kumuunga mkono.

Ridhiwani pia ameahidi kushirikiana na wanachalinze katika kutekeleza yote yaliyofanywa na wabunge waliotangulia lakini pia amewataka wakazi wa Chalinze kupuuza hoja inayotolewa na mgombe wa Chadema inayodhihaki kuwa yeye sio mkazi wa Chalinze. Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chadema Matayo Torongey alinukuliwa akisema kuwa Ridhwani hawezi kugombea Ubunge Chalinze kwa kuwa sio mkazi wa Jimbo hilo.

Aliongeza kuwa ili kuwahakikishia wakazi wa Chalinze maendeleo inatakiwa kwa wagombea kutangaza sera zinazotekelezeka na kuacha kutoa kauli zenye nia ya kuwapumbaza wakazi wa Chalinze.

Alisema kuwa hatotaka kutumia muda wake kufanya kampeni za kiubabaishaji kuanza kurumbana na kukejeli kwa kuwa amekuwa katika misingi mizuri ya kisiasa. Alisema hajatokea chumbani kugombania Ubunge badala yake amekuwa katika misingi ya kisiasa tangia mdogo na amechukua uamuzi wa kuingia katika siasa kwa lengo la kusaidia wananchi.

Alisema kuwa kero kubwa inayowakabili wakazi wa Chalinze ni kukosekana kwa maji ya uhakika, kero ambayo kwa sasa inatatuliwa kwa kuanzishwa kwa mradi wa maji ya uhakika. Aliongeza kuwa pia kuna tatizo kubwa la ukosefu wa huduma bora za afya uhakika za afya kwa wakazi wa eneo la Chalinze. "Najua awali wakazi wa eneo la Chalinze walikuwa wachache sana na kwa sasa kuna ongezeko kubwa la wakazi wa Chalinze hivyo hata mahitaji nayo yanaongezeka"alisema Ridhwani.

Aliongeza kuwa ongezeko hilo limepelekea kuongezeka kwa uhitaji wa huduma mbalimbali kama hizo za  kijamii na kuongeza kuwa akiwa Mbunge atatatua kero hizo."Watu wanadhania kuwa mimi nimetokea chumbani kuja kwenye siasa hapana yani tena hata sio kwa sababu ya kuwa mimi ni mtoto wa Rais ndio nimeona ngoja nije kuuza sura huku sio, ila ni kwa sababu nimekulia katika mazingira haya na ninaona kuwa ni wakati wa kutatua kero za wakazi wenzangu wa huku"alisema Ridhiwani.

Kuhusiana na tatizo la migogoro katika jimbo hilo alisema kuwa anaona kuwa analo jukumu kubwa la kuendelea kushiriki katika kutatua kero zao ambazo CCM kwa muda mrefu imekuwa ikifanya hivyo. Alisema kuwa
atakuwa na haki ya kupata mikosi iwapo akipuuzia kutatua kero ya muda mrefu ya wafugaji na wakulima.

Ridhwani anatarajia kuzindua rasmi kampeni yake Jumamosi ijayo katika jimbo la Chalinze. Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Chalinze unafanyika kufuatia kifo cha aliekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Said Bwamdogo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...