Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, September 6, 2014

Coastal Union kutambulisha wapya Coastal Day


http://www.gushit.com/files/bookmark_photos/29e2087425L.jpg

KLABU ya Coastal Union ya Tanga kesho inatarajiwa kutambulisha wachezaji wote waliosajiliwa kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara unaotazamiwa kuanza Septemba 20 mwaka huu.

Utambulisho huo utafanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga katika siku maalum ya Coastal 'Coastal Union Day' ambayo hufanyika kila mwaka inapofika Septemba 7.
Katika utambulisho huo Coastal maarufu kama Wagosi wa Kaya wataumana na timu iliyorejea Ligi Kuu Polisi Morogoro.
Ofisa Habari wa Coastal Union, Oscar Assenga amesema kuwa maandalizi ya kuelekea utambulisho huo yamekamilikwa kwa asilimia kubwa.

Assenga amesema katika kuelekea siku hiyo maalumu kwa timu hiyo wataangalia uwezekano wa kucheza na timu itakayotajwa baadae baada ya mazungumzo kumalizika.

"Siku hii itakuwa ni maalumu sana kwa timu yetu tunatarajia tutaweza kufanya jambo hilo kwa wanachama,wapenzi na mashabiki wetu ili waweze kufahamu kikosi chao kabla ya kuanza msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara"

Akizungumzia maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa ligi kuu, Assenga amesema kuwa maandalizi kwa timu hiyo yanaendelea vizuri kwa wachezaji kufanya mazoezi asubuhi na jioni.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...