Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, October 10, 2014

BENKI YA POSTA YAZING'ARISHA TASWA FC NA TASWA QUUENS


Meneja mahusiano mwandamizi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Noves Moses (kushoto) akimkabidhi jezi nahodha wa timu ya netiboli ya waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa Queens) Imani Makongoro (Kulia) katika halfa fupi iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo jana. Katikati ni Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary . Picha/Mpigapicha wetu
*****************************************
Na Mwandishi Wetu, Dar
Benki ya Posta Tanzania (TPB) imeendelea kuisadia  timu ya   Waandishi wa habari za  michezo nchini (Taswa SC) baada ya kuikabidhi vifaa vya michezo kwa ajili ya kutumika katika mashindani na michezo mbali mbali ya kirafiki.
Benki hiyo imekabidhi seti za jezi kwa timu hizo zikiwa na jumla ya thamani ya Sh1,180,000 kwa timu ya mpira wa miguu maarufu kwa jina la Taswa FC na timu ya netiboli ambayo pia inajulikana kwa jina la Taswa Queens.
Akizungumza katika makabidhiano hayo, Meneja mahusiano mwandamizi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Noves Moses alisema kuwa msaada huo ni sehemu ya shughuli za benki kijamii na kutambua mchango mkubwa wa waandidshi wa habari hapa nchini.
“Waandishi wa habari wameonyesha mfano mkubwa kwa kucheza soka na netiboli, pia niliona mnafanya mazoezi ya ngumi chini ya bondia Thomas Mashali, huu ni mfano wa kuigwa na ndiyo maana tumevutiwa na utendaji na maendeleo yenu,” alisema Noves.
Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary aliishukuru TPB kwa kuendelea kuwakumbuka na kuahidi kutumia jezi hizo kwa kushinda mechi na wala si kutoka sare au kufungwa.
“Tunajivunia uwepo wa Benki ya Posta kwa kuthibitisha kuwa ni benki halisi ya Watanzania, nachukua fursa hii kuwaomba Watanzania kufungua akaunti zao katika benki hii na vile vile kuomba wadau wengine kufuata mfano wao kwa kuisaidia Taswa SC ili iweze kufanikisha ziara zake,” alisema Majuto.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...