Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, October 22, 2014

MADAWA YA KULEVYA YAKAMATWA DAR ES SALAAM



 

 


GODFREY NZOWA(Kamishina msaidizi Mwandamizi kitengo cha kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya) akionyesha baadhi ya madawa yaliyokamatwa.
 
kuwakamata na kilo saba za Dawa za Kulevya aina ya Heroin,zinazodhaniwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 300 usiku wa kuamkia Jumanne hii.
Watu hao wamekamatwa maeneo ya Magomeni jijini Dar es Salaam,usiku wa kuamkia Jumanne hii.
Wafanyabiashara wanaoshikiliwa na Kitengo hicho ni Mwalami Mohamed Chonji,Mariki Zuberi,Taka Adam,Rehan Musso na Abdul Abdallah ambao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Kamishina msaidizi Mwandamizi wa Kitengo hicho,Godfrey Nzowa amesema,kukamatwa kwa watu hao kunafuatia taarifa kutoka kwa raia wema waliowatilia shaka watu hao.

Aidha,kamishna Nzowa ameendelea kuwataka wananchi kuachana na Biashara hiyo haramu,ikiwa ni pamoja na kutoa wito kwa wakulima wanaozalisha bangi kuacha mara moja ,kwa kuwa zao hilo ni miongoni  mwa dawa za kulevya.Zaidi ya kilo mia tatu za Heroin zimekamatwa na kitengo  hicho tangu kuanza kwa mwaka huu.Hali hiyo inayopunguza kasi ya biashara hiyo hapa nchini.
 
 
Baadhi ya Dawa za kulevya zilizowahi kukamatwa na GODFREY NZOWA

GODFREY NZOWA(Kamishina msaidizi Mwandamizi kitengo cha kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya)

Dawa za kulevya  zilizokamatwa leo Magomeni aina ya Heroin kilo saba zenye thamani ya shilingi Bilioni 300 

Dawa za kulevya  zilizokamatwa leo Magomeni aina ya Heroin kilo saba zenye thamani ya shilingi Bilioni 300 

Mizani iliyokuwa inatumika kupimia Dawa za kulevya.

Kifaa kimojawapo ambacho wamekamatwa nacho watuhumiwa hao wa Dawa za Kulevya.

Dawa za kulevya  zilizokamatwa leo Magomeni aina ya Heroin kilo saba zenye thamani ya shilingi Bilioni 300 

GODFREY NZOWA(Kamishina msaidizi Mwandamizi kitengo cha kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya) akionyesha baadhi ya dawa za kulevya yaliyokamatwa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...