Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, November 6, 2014

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAZINDUA MPANGO KABAMBE UNAOITWA TUTOKE NA SERNGETI NOVEMBA 5-2014 JIJINI DAR ES SALAAM

unnamedMkurugenzi wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti, Ephraim Mafuru, (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari  Makao Makuu ya B Pesa Novemba 5, 2014 jijini Dar es Salaam wakati akizindua  shindano lijulikanalo Chini ya kizibo ( Tutoke na Serengeti), ikishirikiana na B Pesa, ambampo washindi watapelekwa Mbuga za wanyama (wakwanza kulia), Meneja masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti, Allan Chonjo (wapili kushoto), ni Mkurungezi mkuu wa B. Pesa, Robert Boniface, (wakwanza kushoto), Meneja wa Mendeleo ya Biashara, Salil Abbas. unnamed2Meneja masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti, Allan Chonjo (kushoto) akionyesha moja ya zawadi kwa waandishi wa habari zitakazo shindaniwa. unnamed3Meneja wa Mendeleo ya Biashara, Salil Abbas, akielezea huduma mpya ya kutuma fedha ambayo inashirikiana na benki mbalimbali nchini ikiratibiwa na Benki Kuu (BOT) lengo likiwa ni kurahisisha utoaji na utumaji wa fedha katika maeneo mbalimbali.
………………………………………………………………
KAMPUNI ya bia ya Serengeti kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager imezundua mpango kabambe unaoitwa Tutoke na Serengeti na kuwazawadia wateja wake kwakuwapa fursa ya kufaidi utalii wandani kwakuwapeleka kwenye mbuga za wanyama .Promosheni hiyo inalenga kuwafikia wateja wapatao milioni 20 ambao watapata fursa ya kujishindia fedha taslimu na zawadinyingine nyingi.
 Akizungumza jijini Dar es Salaam Novemba 5,2014 wakati akizindua shindano la kuwazawadia watanzania  kwa kuwapa fursa mbalimbali  pamoja na zawadi ambazo kwa ujumla zinagharimu Sh bilioni 1.2. Mkurugenzi Masoko wa  Kampuni ya Bia ya Serengeti, Ephraim Mafuru. Alisema.
 Katika kuendesha shindano hilo, kampuni hiyo imeshirikiana na wataalam wa teknolojia B-pesa ambapo washindi watapata fursa ya kulipwa fedha zao kupitia mfumo huo.
 Kuhusu hifadhi za taifa, alisema kupitia shindano  hilo watanzania  takriban milioni 20, watapata fursa ya kufaidi utalii wa ndani kwa kupelekwa katika mbuga za wanyama  na kuweza kuitangaza Tanzania na vivutio vilivyomo  popote watakapokuwa.
 Alisema Tanzania ina maliasili nyingi ambazo kwa hakika wapo watanzania wasiokuwa na uzalendo wa kuzitembelea na kujionea fahari  ya nchi yao jambo ambalo hubaki huwafanya wengine kuona kama wanaotakiwa kufanya hivyo ni watalii wan je ya nchi peke yake.
 Kuhusu shindano hilo alisema linalojulikana kama “tutoke na Serengeti” na washindi watajishindia zawadi fedha taslimu zenye thamani y ash milioni 100 ambazo zimegawaywa katika mafungu y ash 5000 na kwa mshindi atakaetembelea mbuga za wanyama atapata fursa ya kwenda na marafiki watano wakigharamiwa kila kitu.
 “Kwa kupitia kinywaji cha Serengeti washindi watapata babj sita aina ya limo zenye uwezo wa kubeba abiria saba zikiwa na vifaa vya B-pesa kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali,” alisema na kuongeza kuwa kila wiki mshindi atatangazwa katiak shindano hilo litakalodumu kwa miezi mitatu.
 Kuhusu B-Pesa, Meneja wa Mendeleo ya Biashara, Salil Abbas alisema ni  huduma mpya ya kutuma fedha ambayo inashirikiana na benki mbalimbali nchini ikiratibiwa na Benki Kuu (BOT) lengo likiwa ni kurahisisha utoaji na utumaji wa fedha katika maeneo mbalimbali.
 Alisema kutokana na kukua kwa uchumi nchini  kunasababisha kukosekana kwa usalama wa fedha hivyo kwa kutumia huduma hizo kutawezesha kila mwananchi kuwa huru popote awapo kutumia fedha yake kwa njia iliyo salama kwake.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...