Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, December 25, 2014

WAZIRI UMMY AENDESHA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WASICHAMA WA WILAYA YA MUHEZA MKOANI TANGA


 Mhe Ummy Mwalimu Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais akifungua mafunzo kwa wasichana wa Wilaya ya Muheza juu ya kujitambua na kujithamini katika masuala ya Afya ya uzazi. Mafunzo hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki Wilayani Muheza.

Mhe. Ummy Mwalimu, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia Taasisi ya Maendeleo ya Wanawake wa Mkoa wa Tanga (TAWODE) ameendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo wasichana wa Wilaya ya Muheza, Mkoani Tanga wenye umri  kati ya miaka 10 - 24. Lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha wasichana hao kujitambua na kujithamini katika masuala ya afya  ya uzazi ili kujikinga na mimba na ndoa za utotoni na maambukizi ya VVU/UKIMWI.
 Mhe Ummy Mwalimu Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya kujitambua na kujithamini Wilayani Muheza mwishoni mwa wiki.
 Wasichana wa Wilaya ya Muheza wakifanya majadiliano na mawasilisho katika vikundi juu ya changamoto wanazokumbana nazo katika kipindi cha ujana.
Wasichana wa Wilaya ya Muheza wakifanya majadiliano na mawasilisho katika vikundi juu ya changamoto wanazokumbana nazo katika kipindi cha ujana.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...