Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, August 13, 2015

PETER MUHUNZI WA TEFA APETA RUFAA YAKE MUHIBU KANU AONDOLEWA



Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya DRFA, Advocate Rashid Saadallah (katikati) akiongea na wandishi wa habari kuhusu maamuzi ya rufaa za wagombea wa nafasi mbalimbali za uchaguzi wa Chama cha Soka Temeke (TEFA) jana kwenye ofisi za DRFA jijini Dar es Salaam. Kulia ni katibu wa kamati hiyo Fahad Katanga na kushoto ni msemaji wa DRFA, Omar Katanga. (Picha na Rahel Pallangyo)

MWENYEKITI wa TEFA, Peter Muhunzi na Sizza Chenja wameshinda rufaa baada ya kuwekewa pingamizi kwenye mchakato wa uchaguzi wa Chama cha Soka mkoa wa Temeke. (TEFA)
Akitoa maazimio ya Kamati ya Uchaguzi ya DRFA,Mwenyekiti wa Kamati, Advocate Rashid  Saadallah, alisema kamati yake ilipitia mapingamizi yake kwa makini na kina kwa kufuata katiba ya TEFA, DRFA na ya chama mama ambacho ni TFF na kutoka na maamuzi ambayo hata hivyo alikiri kama mgombea hataridhika anaweza kukata rufaa kwenye ngazi nyingine ambayo ni TFF.
“Peter Muhunzi ambaye anagombea nafasi ya mwenyekiti wa TEFA, ameshinda rufaa yake baada ya kuthibitisha kigezo cha elimu kwa maana ya kumaliza kidato cha nne na Sizza Chenja kamati imempitisha aendelee na mchakato wa uchaguzi baada ya kuthibitisha kuwa ana uzoefu wa kutosha katika uongozi wa mpira wa miguu kama katiba ya TEFA Ibara ya (31)(1)(j) inavyotaka”, alisema Saadallah
Pia alisema Rashid Salim, ambaye pia anagombea nafasi ya Mwenyekiti -ameshindwa kuleta vielelezo kuthibitisha uzoefu wake katika masuala ya mpira kama Ibara ya 31(1)(j) inavyosema pia Aziz Mohamed Khalfan, kamati imegundua kwamba alienda kwenye mchakato wa uchaguzi akiwa hana sifa kwa sababu alifungiwa na kamati ya nidhamu na usuluhishi ya kutokushiriki au kujihusisha na mpira kwa muda wa miezi kumi na mbili (12) na TEFA.
Saadallah alisema kwenye nafasi ya Makamu wa kwanza wa Mwenyekiti, Shufaa Jumanne amepitishwa aendelee na mchakato wa uchaguzi baada ya kuridhika na uthibitisho wa uzoefu wa zaidi ya miaka mitatu katika uongozi wa soka Daudi Mumbuli, kamati inaitupilia mbali rufani baada muweka pingamizi kushindwa kutokea mbele ya kamati kuthibitisha madai yake.
Naye Omary Kapilima ambaye anagombea makamu wa kwanza wa Mwenyekiti  ameondolewa baada ya kushindwa kuleta cheti cha kidato cha nne kinachotambulika na Baraza la Mitihani la Taifa yaani (NECTA) ili kukidhi kigezo cha elimu kama inavyotakiwa na Ibara ya 31(1)(b) ya katiba ya TEFA japo  kathibitisha uzoefu wa uongozi wa mpira na Salehe Mohamed kamati inamuengua katika mchakato wa uchaguzi kwa kushindwa kuthibitisha kiwango chake cha elimu kwa  kushindwa kuleta cheti cha kidato cha nne(Academic Certificate) kama inavyotakiwa na Ibara ya 31(1)(b) ya katiba ya TEFA pia Bakili Makele ambaye alikuwa anagombea makamu wa pili ameenguliwa kwa kigezo hicho cha elimu kwani amekiri kwamba elimu yake ni ya darasa la saba
 Amack Nabola ambaye anagomea Ujumbe wa soka la wanawake na vijana ameenguliwa katika mchakato kwa kukosa sifa ya elimu ya kidato cha nne kama ibara ya 31(1)(b) ya katiba ya TEFA inavyotaka lakini Fikiri Magoso ambaye anagombea mjumbe wa kamati ya Utendaji amepitishwa kugombea nafasi hii kwa sababu anakidhi vigezo kwa kuwa na cheti cha darasa la saba kama katiba ya TEFA anavyomtaka mgombea wa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji kuwa na elimu isiyo chini ya darasa la saba.
Mgombea Muhibu Kanu ambaye alikuwa nagombea nafasi mbili, ya makamu Mwenyekiti na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji kamati imemuengua kwa sababu  ni kinyume cha kanuni za uchaguzi za TFF za mwaka Ibara 10(9) ambayo inakataza mgombea kugombea nafasi zaidi ya moja.
Pia Saadallah alisema kamati yake imefanyia kazi pingamizi la ambazo kikatiba na kanuni kwani zile za matumizi mabaya ya fedha na ubadhirifu, kamati haina mamlaka ya kuyatolea maamuzi hivyo yanapelekwa kwenye kamati ya maadili ya DRFA.
 
 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...