Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, April 6, 2016

SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO) LATOA UFAFANUZI KUHUSU MALIPO YA GHARAMA ZA UMEME NCHINI



 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),Decklan Mhaiki (kulia) akizungumza na waandishi (hawapo pichani) Dar es Salaam kuhusu malipo ya sasa ya gharama za Umeme nchini.Mwengine ni Kaimu Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Wateja,Leila Muhaji.
 Kaimu Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Wateja,Leila Muhaji.akiwakaribisha waandishi kwenye mkutano.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),Decklan Mhaiki (katikati) akizungumza.Wengine ni  Kaimu Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Wateja,Leila Muhaji (kushoto) na Katibu wa Mkurugenzi Mtendaji,Pius Gaspar.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),Decklan Mhaiki(kushoto) akizungumza na waandishi.Mwengine ni  Katibu wa Mkurugenzi Mtendaji,Pius Gaspar.
  Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa kazini.

KESI YA KUPINGA MATOKEO YA UBUNGE JIMBO LA VUNJO,MREMA AKUBALI YAISHE

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

MBUNGE wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia (TLP) ameshinda kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia chama cha Tanzania Labour (TLP)  Augustine  Lyatonga Mrema .

Mbatia ameshinda kesi hiyo baada ya upande wa mlalamikaji (Mrema) kuamua kufuta shauri hilo kwa hati maalumu iliyowasilishwa katika mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi huku akikiri kumtambua Mbatia kama mbunge halali wa jimbo hilo.

Mbali na utambuzi huo Mrema pia amekanusha maelezo pamoja na ushahidi wake aliowasilisha mahakamani hapo dhidi ya Mbatia,wananchi wa jimbo la Vunjo pamoja na taasisi mbalimbali zikiwemo za kidini ambazo zilitajwa mahakamani hapo wakati wa ushahidi wake.

Ukiwasilisha hoja mahakamani hapo mbele ya Jaji wa mahakama kuu Lugano Mwandambo , upande wa mlalamikaji ukiongozwa na wakili January Mkobogho ulieleza kuwa pande mbili katika shauri hilo wamefikia makubaliano nje ya mahakama.

 Wakili Mkobogho aliiomba mahakama kuona makubaliano hayo ambayo yako katika maandishi kama alama kwa mujibu wa makubalinao waliyoafikiana baada ya kuingizwa na kupokelewa mahakamani hapo kama madai.

 Alisema kwa kuwa kesi hiyo ya uchaguzi ikiwa na maslahi mapana ya umma na kwa kuwa mlalamikiwa wa pili na watatu waliunganishwa kwenye shauri hili kwa mujibu wa sheria aliomba kila upande ubebe gharama zao.

Wakili Mkobogho alieleza kuwa kutokana na pande  zilizokuwa zinakwaruzana  wameamua kukaa na kumalizana wenyewe na kwamba haoni sababu za mlalamikiwa wa pili na watatu kutokubeba gharama zao wenyewe.

Jopo la mawakili sita wa upande wa utetezi ukiongozwa  na wakili , Mohamed Tibanyendera uliileza mahakama hiyo kwamba wanaungana na mtoa maombi kwa maslahi ya umma na kwamba wanakubali kila upande kubeba gharama zake.

Wakili mkuu wa  serikali Mark Muluambo akisaidiana na wakili wa serikali Grayson Orcado , alisema wamesikia pande zote na wameafiki kuhusiana na uamuzi huo kutokana na kesi hiyo kuwa na maslahi kwa umma.

Alisema upande wao hauna pingamizi na maamuzi hayo na kwamba wamekili kupokea nakala na wataisoma na kuipitia vizuri, na kutokana na mlalamikiwa wa pili na watatu walitumia gharama katika kesi hiyo waliiomba mahakama  walipwe nusu ya gharama hizo. 

Baada ya kusikiliza maelezo ya pande hizo mbili Jaji Mwandambo alieleza kupata maelezo kuwa mlalamikaji amekiri kwamba kesi hiyo hainafaida yeyote kwa wana Vunjo na kwamba amekubali kuwa tuhuma zake zote alizokuwa nazo juu Mbatia na watu wote aliokuwa anawahusisha na kesi hiyo kuwa amezitengua .

Jaji Mwandambo alieleza kuwa mlalamikaji  pamoja na yote aliyoyasema  pia amekiri kuwa mbunge wa sasa wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia alichaguliwa kwa  kura halali na alipata kura nyingi dhidi yake.

Nje ya mahakama Wakili Tibanyendera alisema haikuwa kazi rahisi kufikia maridhiano haya na kwamba ushawishi mkubwa umefanyika baada ya Wakili anyemtetea Mrema kumueleza ukweli mwenendo wa shauri hilo.

“Tumefanya kazi ya kuwashawishi wateja wetu ,Mrema amekiri katika maandishi yaliyosajiliwa leo mahakamani baada ya kuona kwamba kesi hii haina faida kwa wana vunjo,amekiri na kutengua tuhuma zake zote alizotoa dhidi ya Mbatia,wafuasi wake na taasisi nyingine.”alisema Tibanyendera.

“Hoja kubwa ilikuwa ni kupinga matokeo ya Ubunge,Mrema kwa maandishi amekiri kwamba Mbatia alichaguliwa kihalali na akapata kura nyingi kihalali,hayo yamo katika amri wa mahakama,”alisema Tibanyendera.

Akizungumza mara baada ya kufikiwa kwa uamuzi huo Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia alisema Chama chake kina aamini katika itikadi za utu na kwamba amemsamehe na hata dai gharama za kesi hiyo.

“Tungeweza kumdai Mrema gharama kubwa,tangu kuletwa kwa kesi hiyo mahakamani,mimi sitamdai Mrema hata senti moja,nimemsamehe Mrema kwa sababu ni mpiga kura wa jimbo la Vunjo,nisingependa kuona anadidimia zaidi lazima ni mlee vizuri mzee wngu Mrema,”alisema Mbatia.

“Gharama za mawakili talipia asilimia 50 za mawakili wa upande wetu,Mrema amekubali kulipa sehemu ndogo ya malipo ya mawakili wetu, tungeendelea tungeweza kuuza hata nyumba zake, sasa atalipa Milioni 40 na tayari kwa hatua ya kwanza mawakili watapewa Mil 15 ambazo tayari ziko mahakamani,mwezi ujao atalipa Mil 15 na kabla ya mwezzi wa sita atalipa Mil 10 “aliongeza Mbatia.


 Mbatia aliyekuwa amengozana na mawakili wake pamoja na baadhi ya wafuasi wa chama cha NCCR-Mageuzi  alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi wa jimbo la Vunjo waliokuwa wakifuatilia kesi hiyo .

“Niwashukuru wananchi wa jimbo la Vunjo kwa ushirikiano  na muda mwingi uliopotea kwa ajili ya kufuatilia kesi hii ,yapo mengi ambayo tulitakiwa kuanza kuyafanya lakini muda mwingi tulitumia katika kushughulikia shauri hili “alisema Mbatia.

Upande wa utetezi katika shauri hilo ulikuwa ukiongozwa na Mawakili Mohamed Tibanyendra, Faith Sadala ,Youngsevior Msuya na Mike Kavala huku Mawakili wa serikali wakiwa ni Mark Mluambo Helen Mwajage na Lilian Machange.

Katika uchaguzi huo Mbatia alitangazwa mshindi kwa kupata kura 60,187 huku Mrema akiambulia kura 6,416, na mgombea wa CCM, Innocent Shirima, kura 16,097.

BOSS WA RT AULA KIMATAIFA

Rais wa Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF) Lord Sebastian Coe (kushoto) akipeana mkono na Rais wa Shirikisho la riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

SHIRIKISHO la mchezo wa Riadha Duniani (IAAF) limemteua Rais wa Shirikisho la Riadha nchini (RT) Anthony Mtaka kuwa miongoni mwa wajumbe wanaounda kundi la ushauri wa mikakati ya mawasiliano la shirikisho hilo.


Rais wa IAAAF ,Lord Sebastian Coe alitangaza uteuzi huo hivi karibuni ambapo wajumbe wengine ni Abrahamson Alan wa Marekani, Rodan Joe Junior ,Sierra  Calixto  ,,Karamarinov  Dobromir  kutoka  Bulgaria na Rochdi Souad  wa Ufaransa.


Akizungumza kuhusu uteuzi huo Mtaka ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Simiyu alisema amepokea uteuzi huo kwa furaha kutokana na kuwa ni nafasi ya juu katika sekta maarufu ya michezo katika ngazi ya kimataifa.


“Nimefurahishwa na uteuzi huu hasa ukizingatia nimeteuliwa nikiwa rais wa shirikisho la riadha mwenye umri mdogo kuliko wote kwa sasa takuwa na fursa ya kujifunza mambo mengi mazuri.”alisema Mtaka.


Alisema uteuzi huo ni faida kubwa kwa maendeleo ya michezo katika taifa letu, hasa kipindi hiki ambapo serikali ya awamu ya tano inapoandaa mkakati wa kuiweka sekta ya michezo kuwa sehemu kubwa ya ajira.


Mtaka alisema Tanzania itapata nafasi pana zaidi ya kuwakilishwa katika mikutano mikubwa ya mchezo wa riadha duniani (Decision Making) eneo ambalo linatoa fursa kubwa kwa maandalizi ya mashindano makubwa yajayo baada ya mashindano ya Olyimpiki yatakayofanyika katika jiji la Rio de Jeneiro mwaka huu.


“Taifa litarajie uwakilishi wenye tija, sababu mimi nimeteuliwa kati ya wajumbe nane  ambao kila mmoja wao anawakilisha eneo kubwa, hivyo kama nimepewa dhamana ya kuiwakilisha bara zima la Africa, kwa vyovyote nitaweka maslahi ya nchi yangu mbele bila kuathiri utendaji wa jukumu nililopewa.”alisema Mtaka.


“ Uteuzi wangu ni sifa kwa taifa zima, sifa ambayo itafufua mtazamo mwema ulioonyeshwa na wanariadha wakongwe walioiletea taifa sifa kama Filbert Bayi, Suleiman Nyambui, Gidamis Shahanga, Juma Ikangaa bila kumsahau Mzee John Stephen Akhwari aliyeshiriki Mexico City Games 1968.”aliongeza Mtaka.


Aidha Mtaka alisema uteuzi huo umeongeza hamasa ya kuwekeza maradufu katika kambi ya timu ya taifa ya riadha iliyopo katika hosteli ya Chuo cha misitu cha FITI kilichopo West Kilimanjaro wilayani Siha na Arusha.

FAHAMU MAMBO TISA KUHUSU UKATILI KWA WATOTO

Afisa wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Asha Sarota akiwasilisha mada katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro. Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuliwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto.


Mtangazaji Dominic Maro kutoka Redio Huruma akichangia mada katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro. Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuliwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto.


 Mtangazaji Said Fakhi kutoka Redio Saut ya Quran akichangia mada  katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro. Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuliwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto.

Kutoka kushoto ni Emmanuel Buttorn, Rose Minja (Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Watoto) na Christopher Mushi wote kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro. Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuliwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto.
  .


   Mratibu wa kipindi cha Walinde watoto Neema Kimaro   na Kimela Billa mwandaaji wa kipindi cha Walinde Watoto wakizungumza na waandishi wa habari.katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro. Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuliwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto.

 Tabu Salum kutoka redio ya Sauti ya Quran akichangia mada katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro. Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuliwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto.

 Waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto wakijadiliana mara baada ya mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro. Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuliwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto.
Mambo 9 muhimu ya kufahamu kuhusu Ukatili kwa watoto
Tatizo la Ukatili dhidi ya watoto, linaongezeka siku hadi siku, na kuleta athari mbalimbali za kimwili, kiakili, (kisaikologia) na kiafya kwa watoto. Watoto wanaumizwa, kubakwa, kunajisiwa, kutelekezwa, kusafirishwa kibiashara na kufanyishwa kazi za hatari zinazoathiri afya zao. Matendo haya ya kikatili hayakubaliki kabisa. 
Yafuatayo ni mambo 9 muhimu ya kufahamu kuhusu ukatili kwa watoto:
1.    Aina za ukatili 
Ukatili dhidi ya watoto upo wa aina nyingi. Ukatili wa Kijinsia, ni vitendo au maneno yanayoweza kusababisha madhara kwa mtu au kundi la watu kutokana na maumbile yao. (Mf: kuguswa bila ridhaa, jaribio la kubaka/kubaka, kulazimisha kufanya ngono n.k). Ukatili wa Kimwili ni kama kupigwa, kusukumwa, au kutishiwa kuuwawa kwa silaha. (Mf: kuonyeshwa kwamba hutakiwi, vipigo vya mara kwa mara) na Ukatili wa Kiakili/Kisaikolojia, kutelekezwa, kubaguliwa, kutishwa. (Mf: kuitwa majina mabaya, kunyimwa huduma za msingi, kufanyishwa kazi ngumu n.k)
2.    Wahusika wa Ukatili dhidi ya watoto 
Utafiti wa Ukatili dhidi ya Watoto Tanzania ulifanyika mwaka 2009 na uliongozwa na Kikosi Kazi kinachojumuisha Sekta mbalimbali za Serikali, Asasi za Kiraia na Wadau wa Maendeleo. Katika utafiti huo ilionekana kuwa ndugu  wa karibu kama mjomba, baba, walezi na walimu ndio wanaosababisha ukatili dhidi ya watoto.  Kwa kuona hivyo, Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wakaona umuhimu wa kuanzisha mpango wa kuelimisha jamii kuzuia ukatili dhidi ya watoto. 
3.    Nini kifanyike kupunguza ukatili kwa watoto
Wananchi wote kwa ujumla wana jukumu la kuhakikisha kwamba wanawalinda watoto. Wazazi / walezi wanapaswa kujua watoto wao walipo na wanachokifanya kila wakati na kuhakikisha usalama wa mahali watoto wanapopenda kutembea mara kwa mara. Watoto wapewe moyo kuripoti vitendo mbalimbali vya ukatili. 
4.    Umuhimu wa kituo cha huduma ya simu kwa mtoto - namba 116
Kituo cha huduma ya simu kwa mtoto ni muhimu katika mifumo ya ulinzi wa mtoto nchini. Ni sehemu pekee ambayo mtoto au Mzazi/Mlezi anaweza kupiga simu na kutoa taarifa za ukatili kwa siri na kupata huduma ya ushauri nasaha na rufaa kwa msaada zaidi kwa mujibu wa tatizo lolote linalohusu ukatili dhidi ya watoto. PIGA SIMU BURE kwenda namba 116 kutoa taarifa za ukatili dhidi ya watoto. 
5.    Uchumi na Familia
Familia zikiwa na hali ngumu ya kiuchumi husababisha ugomvi kati ya wanafamilia na hii huweza kupelekea kutelekezwa kwa watoto au kuwatenga watoto na familia, jambo ambalo litaongeza hatari ya ukatili na unyanyasaji wa watoto. Vilevile ugumu wa maisha ni kisababishi cha watoto wanaofanya kazi katika umri mdogo, kuchuuza /kufanya biashara ya watoto, mimba zisizotarajiwa na ndoa za utotoni. Hivyo basi ni muhimu wazazi/walezi kujishughulisha na kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa wanachama wa vikundi  ili waweze kuzalisha mapato ya kusaidia mahitaji ya familia.
6.    Madhara ya adhabu kwa watoto
Kuna madhara mengi sana ambayo yanaweza kuwapata watoto kutokana na kupewa adhabu mbalimbali. Adhabu huleta hasira na chuki ambayo haisaidii kuleta mabadiliko ya tabia. Kadri adhabu inapokuwa kali zaidi ndivyo inavyopelekea mtoto kuwa na matatizo ya kutojithamini, kuwa mhalifu, kupata magonjwa ya akili na kuwa na tabia ya ukatili. Adhabu mara nyingi haitoi mchango chanya kwa maendeleo ya mtoto
7.    Ishara ambazo huonyeshwa na watoto waliofanyiwa ukatili
Ni muhimu kwa wazazi/ walezi kutambua ishara mbalimbali zinazoonyeshwa na mtoto aliyefanyiwa ukatili. Ishara hizo ni kama vile mtoto kutojiamini hata kama anafanya kitu sahihi anakua na hofu kwa sababu tu anahisi anaweza kupigwa. Mtoto kukataa kwenda sehemu ambazo amezoea mf. shule, ukifuatilia kwa ukaribu utakuta kuna mtu anamfanyia ukatili huko au njiani.
8.    Wasikilize kwa makini
Ni muhimu kujijengea mazingira ya kumsikiliza mtoto kwa makini. Unapofanya hivyo ni muhimu ajue kuwa unamsikiliza, aidha kwa kutumia ishara bila maneno; kama vile kuashiria kwa kichwa. Mtazame mara kwa mara kwa mtazamo wa kirafiki.  Unaweza pia kurudia aliyokwambia kwa maneno mengine.
9.    Umuhimu wa vyombo vya habari kupambana na ukatili
Kwa mujibu wa mwongozo wa vyombo vya habari wa kuandika habari za watoto uliochapishwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT), “Watoto wanahitaji uangalizi maalum wa kuwajali na kuwalinda. Wakati wa kuandika habari za watoto, vyombo vya habari vinapaswa kujenga taswira sahihi kwa watoto ili kuwaepusha katika hatari ya kuadhibiwa au kunyanyapaliwa. Watoto ni binadamu wanaohitaji kutambuliwa, kupewa hadhi, utu, heshima na zaidi ya yote kulindwa. Kutokana na ukweli huo, uelewa, umakini na weledi wa uandishi wa habari zinazowahusu wao kwa kuzingatia hali yao na mahitaji yao ni muhimu. Kimsingi vyombo vya habari vinatakiwa kuboresha uandikaji wa habari za watoto na wakati huo huo kulinda usalama wao kimwili na kihisia/jaziba. “
Mambo haya yameibuka katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro.
Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuriwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto.
Redio hizo ni pamoja na Kitulo FM, Radio Maria, Radio Faraja, Boma Hai Radio, Uplands FM, Radio Sauti ya Quran, Kwizera FM na Country FM.
Nyingine ni Bomba FM, Zenji FM, ZBC, Radio Huruma, Ice FM, Radio Jamii Kilosa, TBC Taifa, Dodoma FM, Fadeco Radio, Radio Victoria na Best FM.
Waandishi wa habari wametakiwa kushirikiana na serikali na wadau wengine kuhakikisha kuwa haki za watoto zinatekelezwa hapa nchini.
Ni wajibu wa kila mwananchi kuhakikisha kuwa anawalinda watoto na kuwasadia kukua na kufikia ndoto zao katika jami

Monday, April 4, 2016

NAIBU WAZIRI WA AFYA MAENDELEOYA JAMII JINSIA ,WAZEE NA WATOTO DKT. NASSOR KIGWANGWALLA AZINDUA JENGO LA OFISI ZA T-MARK TANZANIA


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akikata utepe wakati wa kuzindua jengo la ofisi la kampuni ya T-Mark Tanzania, Kulia ni  Mkurugenzi mtendaji wa T-Mark Tanzania,Diana Kisaka na kushoto ni  Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya T Mark, Charles Singili.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akifungua rasmi jengo la ofisi ya T- Mark Tanzania
 Mkurugenzi mtendaji wa T-Mark Tanzania,Diana Kisaka(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo la Ofisi pamoja ja jengo la kuhifadhia mali za kampuni ya T-Mark Tanzania, Kulia ni  Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya T Mark, Charles Singili(katikati)
 Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya T Mark, Charles Singili(katikati)  akizungumza na waandishi wa habari wakatinwa hafla ya uzinduzi wa jengo la ofisi pamoja na ghala la kuhifadhia mali za kampuni.
 Meneja Mradi wa asasi ya T-Mark Tanzania, Doris Chalambo akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa hafla ya ufunguzi wa majrngo ya kapuni ya T-Mark Tanzania
Kikundi cha burudani kikiendelea kutoa burudani wakati wa hafla ya uzinduzi wa majengo ya kampuni ya T-Mark Tanzania
Mkurugenzi mtendaji wa T-Mark Tanzania, Diana Kisaka(katikati) akitoa ufafanuzi kuhusu shughuli wanazozifanya katika kampuni ya T-Mark Tanzania mara baada ya kuwasili kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia) na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya T Mark, Charles Singili.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa T-Mark Tanzania alipotembelea mabanda ya kampuni hiyo wakati wa uzinduzi wa majengo ya kampuni hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kufanya uzinduzi wa majengo ya kampuni ya T-Mark Tanzania
Wafanyakazi wa Kampuni ya T-Mark Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi
Wafanyakaiz wa T-MArk Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa majengo mawili kumalizika
Geofrey Adroph BLOGGER P.O.BOX 24793, Mob: +255 755 274953 /+255 713 363965, Email: pamojapure@gmail.com. Blog: http://www.pamoja.co.tz/ DAR ES SALAAM, TANZANIA

Friday, April 1, 2016

JESHI LA POLISI LAONGEZA MUDA WA KUHAKIKI SILAHA SASA NI MIEZI KITATU NCHI NZIMA

 Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo Makao Makuu ya Polisi, (CP) Nsato Mssanzya (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, kuhusu mchakato wa kuhakiki silaha ambapo jeshi hilo limeongeza muda wa miezi mitatu kwa nchi nzima kuanzia leo.
 Msemaji wa Jeshi Nchini, Advera Bukumbi (kulia), akizungumza na wanahabari wakati akimkaribisha  Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo Makao Makuu ya Polisi, (CP) Nsato Mssanzya kuzungumza na waandishi.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

JESHI la Polisi nchini limeongeza muda wa miezi mitatu kwa ajili ya kutoa fursa kwa wananchi kuhakiki silaha zao kote nchini.

Hayo yalibainishwa na Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo Makao Makuu ya Polisi, (CP) Nsato Mssanzya wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana wakati akitoa taarifa kuhusu kufanyika kwa amani uchaguzi wa marudio wa Urais Zanzibar na uhalifu mbalimbali hasa wa makundi ambao unaonesha umeanza kushamiri.


Kamishna Mssanzya alisema mchakato wa kuhakiki silaha na  kuzisajili na kufanya malipo  katika mkoa wa Dar es Salaam unaendelea vizuri. 

Akizungumzia vitendo vya uhalifu Mssanzya kuwa jeshi hilo limejipanga vizuri kukabiliana navyo hasa uhalifu unaofanywa na mtu mmoja mmoja kwani ule wa makundi wamefanikiwa kuudhibiti kwa kiasi kikubwa

"Hivi karibuni tumefanikiwa kuwakamata watu katika maeneo mbalimbali wanaojihusisha na uhalifu wa kimakundi ambao bado tunaendelea kuwahoji na kufanyiwa uchunguzi" alisema Mssanzya.

Alisema watu hao wamewakamata Mafia na kuwa jeshi la polisi linaendelea kuwafanyia uchunguzi ili waweze kupata taarifa mbalimbali ambazo zitasaidia kuweza kuwatia nguvuni watu wengine.

Alisema pamoja na kuwakamata watu hao jeshi hilo linaendelea kufanya msako katika maeneo yote nchini kuhakikisha vikundi hivyo vinadhibitiwa na kutoa rai kwa wananchi kuongeza ushirikiano ili kuwakamata watu hao.

"Jeshi kama jeshi pekeake aliwezi likakakamata wahalifu bila kupata ushirikiano wa wananchi kwani wengi wao wapo miongoni mwao hivyo wananafasi kubwa ya kuwaona na kutoa taarifa ili waweze kukamatwa," alisema.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)


Thursday, March 31, 2016

KAMATI YA BUNGE, MALIASILI, UTALILI, ARDHI NA MAZINGIRA WAMTAKA WAZIRI LUKUVI KUFUTA HATI MILIKI YA ECO ENERGY


 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Injinia Ramo Makani kulia akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili,Ardhi na Utalii,Meja Jenerali Gaudance Milanzi katikati kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa wa Shirika la Hifadhi za Taifa(TANAPA),Ibrahim Mussa wakati wa ziara ya siku moja ya kamati ya Bunge Maliasili,Ardhi na Utalii kwenye hifadhi ya Taifa ya Saadani,
Wajumbe wa Kamati ya Bunge,Maliasili,Ardhi na Utalii wakiingia kwenye hifadhi ya Taifa ya Saadani jana

 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge,Maliasili,Ardhi na Utalii Atashasta Justus Nditiye akitoa maazimio ya kamati hiyo mara baada ya kuitembelea hifadhi ya Taifa ya Sadani wa kwanza kushoto ni Mjumbe wa kamati hiyo,Marry Chatanda ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe mjini.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Injia Ramo Makani akizungumza wakati wa ziara hiyo

Kaimu Mkurugenzi wa (TANAPA),Ibrahim Mussa akizungumza wakati za ziara ya kamati ya Bunge Maliasili,Utalii na Ardhi Mazingira ilipotembelea hifadhi ya Taifa ya Saadani.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Meja Jenerali Gaudance Milanzi akizungumza wakati za ziara ya siku moja ya Kamati ya Bunge ya Maliasili,Utalii na Ardhi

 Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Tanapa,Mtango Mtaniko akizungumza wakati wa ziara ya kamati ya Bunge Maliasili,Utalii na Ardhi walipofanya ziara ya kutembelea hifadhi ya Taifa ya Saadani
Mjumbe wa Kamati ya Bunge Maliasili,Utalii,Ardhi na Mazingira,Pauline Gekule akiulizwa swali wakati ziara hiyo

MJUMBE wa Kamati ya Bunge,Maliasili,Ardhi na Utalii,Shabani Shekilindi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Lushoto mkoani Tanga akiuliza swali wakati wa ziara hiyo

Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini,Marry Chatanda ambaye pia  ni mjumbe wa kamati hiyo akichangia hoja kwenye ziara hiyo


Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudance Milanzi kulia akiteta jambo na Meneja wa Mawasiliano wa Tanapa,Pascal Shelutete wakati kamati ya Bunge Maliasili,Ardhi na Utalii walipotembelea hifadhi ya Taifa ya Saadani Picha kwa Hisani ya Tanga Raha Blog

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...